- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
DR. GWAJIMA. BAAADA YA CHANJO MUME WANGU ALINITESTI AKAKUTA NIKO FITI
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, nchini Tanzania Dr. Dorothy Gwajima leo amewaacha na hamaki wakazi wa jiji la Mwanza mara baada ya kusema, baada ya yeye kuchanja chanjo ya UVIKO-19, mume wake ametesti 'mitambo' kwake na kukuta yupo 'fiti' kama mwanamke.
Ametoa kauli hivyo leo jijini Mwanza alipokagua jengo la Mama na Mototo katika Hospitali ya Sekou Toure ya Jijini Mwanza.
Amesema chanjo haiathiri kitu chochote katika mwili ndio maana yeye yupo vizuri baada ya kuchanjwa chanjo hiyo na kuhimiza watu kwenda kuchanjwa.
Kumekuwa na taarifa kinzani mbalimbali juu ya chanjo hiyo ya UVIKO 19, moja ni kutoka Serekalini inayohamasisha na kumtaka mwananchi kuchanjwa chanjo hiyo kwa kuwa ni salama na inaokoa maisha, lakini kauli nyingine ni iliyoibuliwa na Askofu Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima ambaye anahubiri kila kukicha kuwa chanjo hiyo Sio salama na Viongozi wengi wa Serekali nchini wanafanya maigizo kwenye kuchanjwa.
Kauli hiyo ya Askofu Gwajima ilimlazimisha Dr. Gwajima jana kuliagiza Jeshi la Polisi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( Takukuru) kumkamata na kumhoji mbunge huyo wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi wa nchi kuhusu chanjo ya Uviko 19.
Askofu Gwajima amekuwa akitoa taarifa za kupotosha kwa makusudi jambo ambalo linaloivuruga wizara yake ya Afya na Serikali ya Jamhuri katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.