Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 7:22 pm

DC KILWA: ZITTO ALIKAMATWA KWA KOSA LA KUFANYA MAANDAMANO BILA KIBALI

Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christoph Ngubiagai, amesema kuwa Jeshi la Polisi linamshikilia kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo Mbunge Zitto Kabwe na Viongozi wengine 6 kwa kosa la kufanya maandamano yasiyokuwa na kibali mjini kilwa.

Ndubiagai amesema viongozi hao pamoja na wafuasi wao walikuwa katika maandamano wakitokea maeneo ya bandarini kuelekea eneo ambalo kiongozi huyo alikamatiwa.

"Na dhamana zao ziko wazi tangu jana sasa ni wao tu, wakamilishe" amesema DC huyo.

Mbali na Zito Kabwe, wengine wanaoshikiliwa ni Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kusini, Selemani Bungala (Bwege) na mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Lindi, Isihaka Mchinjita, wanachama wengine 5.