Home | Terms & Conditions | Help

April 4, 2025, 7:39 am

CHADEMA YAWASILISHA BUNGENI BARUA YA KUWAVUA KINA MDEE UBUNGE

Dodoma. Katibu Mkuu wa chama kikuu cha Upinzani nchini Tanzania Chadema John Mnyika amesema ameshawasilisha Barua ya maamuzi ya Baraza Kuu kuhusu kutupilia mbali rufaa za waliokuwa wanachama 19 wa Chama hicho kwa Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Tulia Ackson.

Wabunge hao ni pamoja na Halima Mdee, Grace Tendega, Agnesta Lambet, esca Kishoa, Ester Bulaya, Ester Matiko, Salome Makamba, Nusrat Hanje, Tunza Malapo, Conchestar Rwamlaza, Naghenjwa Kaboyoka, Hawa Mwaifunga, Stella Fiao, Anatropia Theonest, Asia Mohammed.

Wengine ni Sophia Mwakagenda, Cecilia Pareso, Kunti Majala na Felister Njau, ambao kwa pamoja walivuliwa nyadhifa za uongozi na uanachama mwaka 2020 baada ya kubainika kwenda kinyume na msimamo wa Chadema kula kiapo cha kuwa wabunge wa viti maalumu bila baraka za Chadema.

"Hii ni barua ya pili baada ya ile ya kufukuzwa kwao uanachama na Kamati Kuu mwaka 2020. Spika ni vyema akaheshimu na kutekeleza sasa matakwa ya katiba ya nchi na sheria" amesema Mnyika kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Barua hiyo imewasilishwa leo hii Ijumaa saa 2:42 mchana Mai 12, 2022 na Naibu katibu mkuu wa chama hicho Benson Kigaila kwenye ofisi ya Spika Wa bunge Tulia Ackson.

Aidha Kigaila amesema Barua hiyo pia ameiwasilisha ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi leo mchana Saa 6: 02.

Mchakato wa Rufaa za wabunge hao.

Baraza kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) usiku wa Mei 12 lilitupilia mbali rufaa za waliokuwa wanachama wao 19 na kubariki maamuzi ya kuwafukuza uanachama yaliyofanywa na Kamati kuu ya chama hicho mwaka 2020.

Maamuzi hayo yalifayika usiku wa Mei 12,2022 kwenye kikao cha Baraza Kuu kilichoanza kufanyika Mei 11,2022 katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam lenye ajenda tano na kuhudhuriwa na wajumbe zaidi ya 400 wa chama hicho, wanaotoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Matokeo ni kama ifuatavyo;

*Kanda ya Victoria Wajumbe 44*

-Wanaokubalia wavuliwe uwanachama 42

-Wasiokubali 1

-Wasiofungamana na Upande wowote 1

_*Jumla kura 44*_

*Kanda ya Nyasa Wajumbe 57*

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 57

-Wasiokubalina 0

-Wasifungamana na Upande wowote 0

_*Jumla ya Kura 57*_

*Kanda ya Unguja Wajumbe 22*

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 19

-Wasiokubali 1

-Wasifungamana na Upande wowote 1

_*Jumla ya Kura 22*_

*Kanda ya Pemba 15*

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 12

-Wasiokubali 1

-Wasifungamana na Upande wowote 2

_*Jumla ya Kura 15*_

*Kanda ya Kusini 32*

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 32

-Wasiokubali 0

-Wasifungamana na Upande wowote 0

_*Jumla ya Kura 32*_

*Kanda ya Pwani 47*

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 45

-Wasiokubali 0

-Wasifungamana na Upande wowote 2

_*Jumla ya Kura 47*_

*Kanda ya Kati 44*

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 44

-Wasiokubali 0

-Wasifungamana na Upande wowote 0

_*Jumla ya Kura 44*_

*Kanda ya Serengeti Wajumbe 41*

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 41

-Wasiokubalina 0

-Wasifungamana na Upande wowote 0

_*Jumla ya Kura 41*_

*Kanda ya Magharib Wajumbe 37*

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 37

Wasiokubali 0

Wasifungamana na Upande wowote 0

_*Jumla ya Kura 37*_

*Kanda ya Kaskazini Wajumbe 61*

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 61

-Wasiokubali 0

-Wasifungamana na Upande wowote 0

*Jumla ya kura 61*

*Kamati Kuu*

Wanaokubali wavuliwe uanachama 23

Wasiokubali 0

Wasiofungamana 0

*Jumla ya kura 23*

*Wanaounga mkono wafukuzwe uanachama kura 413*

*Wasiounga mkono kufukuzwa kura 5*

*Wasiofungamana na upande wowote kura 5*

*Jumla ya kura zilizopigwa 423*