- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
BURUDANI: R.KELLY ATOKA GEREZAINI BAADA YA KULIPA SH MILIONI 350
Shirika la habari la Associated Press la nchini Ufaransa limeripoti kuwa Mwanamuziki wa R.n.B wa nchini Marekani R. Kelly ameachiwa kutoka Gerezani baada ya kulipa Kiasi Cha dola za kimarekani $161,633 sawa na Takribani Tsh milioni 354, pesa hizo ni zamatunzo kwa mtoto wake aliyedaiwa kumtelekeza.
R.Kelly mwenye umri wa miaka 52 alishtakiwa na mama watoto wake katika mahakama nchini Marekani siku ya Jumatano na akawekwa ndani kwa maagizo ya Jaji akidaiwa kushindwa kutimiza wajibu wake kama baba kwa mwanae ya matunzo ya mtoto(Child Support)
Mwanasheria wa Kelly, Steve Greenberg alisema kuwa hawawezi kulizungumzia swala la malipo ya matunzo kwa mtoto (child support) kwasababu maelekezo ya jaji katika kesi hiyo.
Kabla ya hapo Mwanamuziki huyo anakabiliwa na kesi lukuki za unyanyasaji wa kingono kwa watoto chini ya Umri wa miaka 18, kesi ambazo zimeshusha heshima yake na ameingia gharama kubwa zaidi mpaka sasa.