Home | Terms & Conditions | Help

November 21, 2024, 4:44 pm

BORIS JOHNSON: KUJADILIANA NA PUTIN SAWA NA KUJADILIANA NA MAMBA MDOMONI WAKE

England (Muakilishi Publisher): Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema kufanya mazungumzo na Rais wa Urusi Vlidamir Putin ni sawa na kujadiliana na "mamba akiwa ameweka mguu wako kwenye taya zake za meno".

Johnson ametoa kauli hiyo hii Aprili 21, 2022 wakati akifanya mazungumzo na waandishi wa habari akiwa kwenye ndege kuelekea India.

Johnson alisema Putin anaweza tu kukubali mazungumzo ikiwa atapata nafasi ya kuongeza nguvu zake nchini Ukraine.

Kauli ya Bw. Johnson inaonekana ni ya kukata tamaa juu ya hatua ya Urus kuivamia Ukraine.

Kiongozi huyo mkuu wa Uingereza ambaye nchi yake ni mwanachama wa Jumuiya ya kujihami ya nchi za Magharibi NATO alionya kuwa kiongozi huyo wa Urusi anaweza kutafuta kuanzisha mashambulizi mapya katika mji mkuu wa Kyiv.

Kuhusu upande wa Ukraine, Johnson alidhani Rais Zelensky alitaka kuona vikosi vya Urusi vikifukuzwa kutoka mashariki mwa Ukraine.

Lakini alifikiria Zelensky angefikiria kuzungumza juu ya Crimea - peninsula ambayo ilichukuliwa na vikosi vya Urusi mnamo 2014.

Kwa vyovyote vile, alisema ni juu ya wananchi kuamua mustakabali wao. "Hakuna kinachopaswa kuamuliwa kuhusu Ukraine bila Ukraine," alisema.