- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
ASKOFU GWAJIMA: SIJALISHWA SUMU NA HAKUNA WAKUNILISHA
Dar es Salaam. Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima, amekanusha vikali taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya Kijamii kuwa amelishwa sumu kutokana na msimamo wake kuhusu kutoikubali chanjo ya Ugonjwa wa Corona.
Askofu Gwajima amesema kuwa hajalishwa sumu, na hakuna mtu wa kumfanyia hivyo.
Kauli hiyo ya Gwajima ameitoa hii leo Ijumapili ya Agosti 8, 2021 wakati akizungumza kwenye ibada kanisani kwake.
Nakwamba, “Wanataka kusingizia watu, labda kusingizia kwamba serikali imeninywesha sumu. Niwahakikishie kwamba hakuna serikali imemnywesha sumu Gwajima kwa kuwa serikali ndiyo inasema chanjo ni hiyari. Hakuna wa kuninywesha sumu na hatotokea" amesema Gwajima
Askofu huyo ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Kawe alizungumzia pia suala la chanjo huku akisema suala la afya ya mtu linapaswa kulindwa na mtu mwenyewe.
“Labda nitoe changamoto kwa wanaojiita watalaam waje walete andiko linaloonyesha kemikali zilizopo kwenye chanjo.
Askofu Gwajima amekuwa akitolea ufafanuzi msimamo wake juu ya chanjo ya Corona akisema kuwa yeye binafsi na familia yake hawatachanjwa chanjo hiyo kwakuwa anaichukulia sio salama kama wanayochanjwa mataifa ya Magharibi na Ulaya kwa Ujumla wake.
Taarifa iliyotolewa jana Agosti 7, 2021 na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Profesa Abel Makubi ilieleza kuwa tangu kuanza kutolewa kwa chanjo hiyo idadi ya watu wanaotaka kuchanjwa imekuwa ikiongezeka siku hadi siku.
Alisema rekodi ya Agosti 7 ilionyesha zaidi ya watu 164,500 walikuwa wamejisajili kwa ajili ya kupatiwa chanjo hiyo katika juma la pili tangu ianze kutolewa kwa watu wa makundi ya kipaumbele.