Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 10:01 am

ACT WAZALENDO: HATUKUMFUKUZA MEMBE KWENYE CHAMA

Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Bi Dorothy Semu, amesema kuwa aliyekuwa Waziri Wa mambo ya njee n Tanzania Bernard Membe, aliondoka ndani ya chama hicho kwa utashi wake mwenyewe na hakufukuzwa na mtu yeyote na kwamba kama atahitaji kurejea tena ndani ya chama basi anakaribishwa.

Kauli ya Bi Dorothy ameitoa hii leo Februari 24, 2021, wakati akifanyiwa mahojiani ya na kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio, ambapo pia ametumia nafasi hiyo kuviomba vyama vingine vya siasa kuhakikisha vinatoa nafasi kwa wanachama wao ambao watakuwa wameiridhisha nao.

"Siasa ni 'dynamic' Bernard Membe tulimpokea na baadaye alijitoa ndani ya chama chetu, hatujutii kumpokea lakini tumejifunza mengi kutoka kwake, unajua kuna vitu vinakuwa ndani ya mtu huwezi kuviona kwa macho", amesema Dorothy.

"ACT Wazalendo tutaendelea kuwa kimbilio la watu wanaotaka kufanya siasa safi, siasa za maendeleo na matendo, Membe akirudi tena anayo haki ya kupokelewa hatukatai wanachama sisi hatukumfukuza aliondoka yeye mwenyewe", ameongeza.