- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
TULIA ACKSON: MAMLAKA YA RAIS NIMAKUBWA, HAYAFANANI NA MUHIMILI WOWOTE
Dodoma. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson amesema kuwa Mamlaka ya Rais ni makubwa sana na hayafanani na ya Kiongozi wa muhimili mwingine wowote hapa nchini.
Aidha Ackson ametumia hafla hiyo kusisitiza kuwa Rais ni Mkuu wa nchi na kwa wale wanaodhani kuwa ni Mkuu wa Serikali waondokane na dhana hiyo.
"Nisisitize jambo moja maana kuna upotoshaji, Rais ni Mkuu wa Nchi, ni Kiongozi wa Serikali, ni Amiri Jeshi Mkuu, kwahiyo yeye uongozi wake haupo sawasawa na Kiongozi yoyote wa Mhimili wowote hapa nchini" amesema Naibu Spika Dr. Tulia Ackson
kazi ya Bunge ni kuishauri na kuisimamia Serikali, hivyo litaendelea kufanya hivyo pamoja na kumpa Rais ushirikiano.
Dkt. Tulia ametoa kauli hiyo Ikulu Chamwino mkoani Dodoma wakati Rais Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwaapisha Viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni.
Kwa upande wa Viongozi walioapishwa, amewataka wakatumie uzoefu wao katika kutimiza majukumu yao ya kila siku na wajitume katika luwatumikia Wananchi.