Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 1:19 am

SPIKA NDUGAI: MBOWE LAZIMA ARUDISHE FEDHA ZA POSHO

Dodoma: Spika wa Bunge wa Tanzania Job Ndugai ameendelea kumkalia kooni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe kwa kumtaka kurudisha Fedha za posho za vikao za wiki mbili alizochukua yeye sambamba na wabunge wenzake wa chama hicho baada ya kujiweka karantini wenyewe.

Kauli hiyo ya Spika Ndugai ameitoa leo Mei 18, 2020 Nyumbani kwake Nzuguni Jijini Dodoma.

“Ni hiyari yako kujifungia ila usichukue fedha za Umma kwamba unakwenda kufanya kazi halafu unatumia fedha kwa matumizi mengine, umechukua posho Bungeni hauendi ni dhambi, ndio maana nikaagiza warudishe Mil 110 za Wananchi,sasa hapo Spika amekosa nini?” amesema leo Spika Ndugai•

“Hata mwandishi ukichukua fedha ya kazi halafu usiende kwa kusema umejiweka lockdown watakushangaa, kuna Wabunge wengine wamerudisha fedha, wengine bado akiwemo Mbowe niombe arudishe, na hiyo fedha lazima itarudi tu, njia gani nitaitumia niachieni mimi”-NDUGA•

“Mbowe alisifia Nchi moja jirani kwamba haina kifo cha corona, Mtu anapokufa Serikali au Bunge limetaka?, kama hakuna aliyekufa huko unaisema Tanzania kwa lipi?, ana ushahidi hawajafa, tukitaka athibitishe?, lazima uelewe takwimu hizo ni kweli au magumashi!”-NDUGAI •

Aidha spika Ndugai amemjibu Mbunge huyo wa Hai kuwa anatakiwa kujiangalia kwanza makosa yake na mapungufu aliyonayo kabla ya kuanza kusema yawenzake.

"Mbowe anasema tumuombee spika sababu hajui atendalo, nimjibu kwamba ondoa boriti kwenye jicho lako kabla haujaona vibanzi vya wenzako, kama utarudi kuomba Ubunge Hai au Moshi mjini unapotaka kukimbilia, wakikuchagua uje uwe mwakilishi kweli usiwe mtoro”-NDUGAI