Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 1:09 am

NEWS: WHO YAKUBALI KUANZA KWA UCHUNGUZI KUHUSU CORONA

Shirika la Afya Duniani WHO hatimaye limekubali kuanzisha uchunguzi kuhusu namna lilivyoushughulikia mzozo wa virusi vya corona, katika wakati ambapo China inaituhumu Washington kwa kukwepa wajibu wake.

China ilitoa shutuma hizo baada ya rais Donald Trump wa Marekani kutishia kujiengua kwenye shirika hilo. Hatua hiyo inakuja wakati maambukizi ya corona ulimwenguni yakikaribia milioni 5.

World should have listened' to WHO on Covid-19, its director says

Mkurugenzi mkuu wa WHO, Dr. Tedros Adhanom Gebreyuses alisema mapambano ya janga hilo ni lazima yawe ya kipaumbele, ingawa maradhi ya COVID-19 yanaendelea kusababisha vifo na kudhoofisha uchumi kote ulimwenguni. Rais Trump alilituhumu WHO kuwa ni kibaraka wa China na limeshindwa kufanya vya kutosha katika kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona.

Idadi ya vifo imezidi kuongezeka katika baadhi ya maeneo, huku Uingereza ikifichua zaidi ya watu 41,000 wamefariki kutokana na maradhi ya COVID-19.

Donald Trump - Schutzmaske (picture-alliance/S. Reynolds)

Siku ya Jumatatu, Trump alitishia kuondoa kwa muda ama moja kwa moja ufadhili kwenye shirika hilo, na China ilijibu kwa kumtuhumu Trump kujaribu kuichafua China na kuivuruga WHO kwa maslahi ya kisiasa.

Urusi pia ilikosoa kitisho hicho cha Trump. Umoja wa Ulaya inayoliunga mkono shirika hilo lilisema huu sio muda wa kunyoosheana vidole.

Nchini Brazil kumerekodiwa vifo 1,179 vya COVID-19 katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita. Hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa idadi ya vifo ya siku moja kupindukia 1,000. Kulingana na wizara ya afya nchini humo, idadi jumla ya vifo imefikia 17,971. Maambukizi mapya katika muda kama huo yalifikia 17,408 na jumla ya watu 271,628 wameambukizwa.