Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 1:31 am

NEWS: WAMACHINGA DAR WAFUNGA BARABARA YA MKUU WA MKOA

Dar es salaam. Wafanya biashara wa Jamii ya Kimachinga katika Soko la Karume wamefunga barabara iliyopo karibu na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla wakishinikiza kuruhusiwa kuendelea kufanya biashara kwenye soko hilo lililoungua usiku wa kuamkia jana Jumapili Januari 16, 2022.

Wamachinga hao wamefunga barabara katika makutano ya barabara ya Uhuru na barabara ya Kawawa Ilala Boma muda mfupi baada ya kuandamana mpaka kwenye geti la Ofisi ya Mkuu huyo wa Mkoa.

Wamachinga Wamedai kwamba wanashinikiza mkuu huyo wa Mkoa atoe tamko la kuwaruhusu waendelee kufanya shughuli zao kwenye soko hilo kama kawaida.

Waliandamana huku wakiwa wanaimba "Tunataka Soko letu" wakiwa wamezingira geti la ofisi hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ng'wilabuzu Ludigija aliwaomba wafanyabishara hao kuwa wavumilivu na kufuata utaratibu uliotangazwa na Serikali kwamba waiachie kamati ifanye kazi kwa siku saba na kutoa ripoti badala ya kuandamana kutaka kushindana na Serikali.

"Mnatakiwa kujiongeza pamoja na kwamba mnadai haki lakini lazima mfuate utaratibu Jana Waziri tuiachie Kamati ifanye kazi na walete ripoti tunaomba kuweni na subira,"aliwasihi