Home | Terms & Conditions | Help

April 9, 2025, 2:19 pm

NEWS: WADAU WA UTALII ARUSHA WAKUBALIANA KUTENGENEZA MWONGOZO

Arusha. Wadau wa Utalii waliokutana jijini Arusha kwa siku mbili wameazimia kutengeneza mwongozo wa kina unaofafanua jinsi ya kuendesha utalii ndani ya janga la ugonjwa wa COVID-19 ambao utawasilishwa kwenye mamlaka zinazohusika katika serikali ili kuurasimisha.

Akisoma maazimio hayo, leo Mei 13, 2020 Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala amesema mwongozo huo utatoa mwelekeo na mwenendo mzima wa kufungua na kuendesha shughuli za utalii nchini katika kipindi hiki ambacho dunia nzima imeathirika na janga hili.