- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: VIONGOZI HASIMU WA AFGHANISTAN WAGAWANA MADARAKA
Hatimaye Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani na hasimu wake Abdullah Abdullah Jumapili wamesaini makubaliano ya kugawana madaraka, na kumaliza mzozo ulioendelea kwa miezi kadhaa hadi kulitumbukiza taifa hilo katika mgogoro wa kisiasa.
Msemaji wa Ghani Sediq Sediqqi, ameandika kwenye mtandao wa Twitter kwamba Abdullah ataongoza Tume ya Kitaifa ya Maridhiano na wanachama wa timu yake watajumuishwa kwenye baraza la mawaziri.
Hatua hiyo imefanikishwa wakati ambapo Afghanistan inapambana na msururu wa migogoro iliyolikumba taifa hilo, ikiwa ni pamoja na kuenea kwa haraka kwa maambukizi ya virusi vya corona pamoja na ongezeko la vurugu zinazofanywa na wanamgambo ambapo watu kadhaa waliuawa katika shambulio la kikatili wiki iliyopita.