- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TRUMP ALIVYOSUSA MKUTANO WAKE NA WAANDISHI WA HABARI
Rais wa Marekani, Donald Trump, hapo jana alifanya mkutano wa kwanza na wanahabari tangu Aprili 27, kuelezea maendeleo ya vita dhidi ya corona.
Hotuba yake ilijaa majigambo kwamba nchi yake inafanya vizuri zaidi duniani katika upimaji wa virusi vya corona.
Majigambo hayo hayakumvutia mwandishi wa kituo cha CBS, Weijia Jiang, raia wa Marekani mwenye asili ya bara la Asia.
Akamuuliza, 'Umekuwa ukijisia tu kwamba Marekani inafanya vizuri kwenye upimaji'. Trump akaitikia, 'Ndiyo'. Jiang akaendelea, 'Hii ina maana gani wakati kila siku wamarekani wanakufa...na lila siku kuna visa vipya'? Trump akajibu, 'Kufa watu wanakufa kila sehemu duniani. Labda hilo swali ungewauliza China. Usiniulize mimi hilo swali. Waulize China. Ukiwauliza China, watakupa jibu lisilo la kawaida'. Halafu akaruhusu mtu mwingine aulize swali.
Lakini yule mdada wa watu akahisi kutotendewa haki, kwamba Trump kamwambia vile kwa sababu anaonekana kama mchina.
Akasema, 'Kwanini ukaniambia hivyo, kunilenga mimi binafsi?
Trump akajibu, 'Nakwambia wewe lakini sijakulenga wewe binafsi. Sijamlenga mtu yeyote binafsi.
Nimesema kwa mtu anayeuliza swali la hovyo kama hilo.
Hapo mdada akaumia zaidi kuambiwa swali lake la hovyo...akataka kuendelea kupamba, lakini Trump akatupia kijiti kwa mwingine.
Aliyekuja kutaka kuuliza swali ni yule aliyeruhusiwa hapo kabla, baada ya mdada wa kichina kujibiwa...lakini kwa kuwa aliendelea kujibizana na Rais, ikabidi yule aliyetakiwa kuuliza, asubiri kwanza.
Jina lake ni Kaitlan Collins, mwandishi wa CNN.
Na sasa ndiyo imefika zamu yake, anataka kuuliza, lakini Trump akamkatalia, na kuruhusu mwandishi mwingine kuuliza swali.
Dada akajieleza kwamba alisharuhusiwa hapo, lakini Trump akamwambia kwamba ni kweli alimruhusu lakini hakuuliza hivyo zamu yake imeshapita.
Akamuita mwandishi mwingine, yule dada akaendelea kukomaa, akata kuuliza swali kwa niaba ya huyo mwingine ambaye alipewa nafasi na Rais Trump.
Trump alivyoona maswali ya mkanganyiko juu yake yamekuwa mengi akakimbia kwa kuwashukuru na kuwaaga.
Imeandaliwa na #Zakazaka