Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 12:52 am

NEWS: SPIKA NDUGAI NA CECIL MWAMBE WASHTAKIWA KWA KUVUNJA KATIBA

Dar es salaam. Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai na aliyekuwa Mbunge wa Ndanda baada ya kujiengua Chadema Cecil Mwambe, kwa pamoja wameshtakiwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania kwa madai ya kuvunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Spika Ndugai, Cecil Mwambe Washtakiwa Mahakama Kuu - Global Publishers

Katika Shtaka hilo pia ameunganishwa ni pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kesi hiyo imefunguliwa na Shirika la Uraia na Msaada wa sheria (CILAO), leo tarehe 20 Mei 2020 kupitia wakili wake John Seko.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Odera Odero, Mkurugenzi wa CILAO, wamefungua shauri baada ya kupata maoni ya Watanzania 3000 waliopinga kitendo cha Spika Ndugai kumrejesha bungeni Mwambe.

Mwambe alikuwa mbunge kupitia Chadema ambapo tarehe 15,Februari 2020, alijiuzulu na kurejea Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hata hivyo, Spika Ndugai alimrejesha bungeni licha ya kujivua uanachama wa Chadema. Shirika hilo linaiomba mahakama kutoa tafsiri juu ya kitendo cha kumruhusu Mwambe kuhudhuria vikao vya Bunge kama mbunge baada ya kujiuzulu. Odero ameeleza, kwa mujibu wa Ibara ya 26(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, inatoa wajibu wa kila raia kuitii Katiba pamoja na Sheria za Jamhuri ya Muungano.