- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS; SIKU 100 ZA RAIS SAMIA ZIMEBEBA UMAHIRI WAKE KATIKA KAZI.
DODOMA; Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu amesema siku 100 za Rais Samia Suluhu Hassan madarakani zimebeba umahiri na dhamira halisi ya matamanio yake katika kuwaletea maendeleo watanzania.
Akizungumza na Mtandao huu Juni 27 jijini Dodoma,Mtaturu amesema Rais Samia ameweka matamanio aliyoyanyo kwa watanzania kwa vitendo kupitia bajeti yake ya kwanza iliyogusa makundi yote.
"Katika bajeti ya 2021/2022 ambayo ni ya kwanza katika utawala wake,tumeona nyongeza ya fedha kiasi Cha Shilingi Bilioni 322 kikielekezwa kwenye kujenga barabara za vijijini kupitia TARURA,hatua hii itawezesha uchumi wa wananchi mmoja mmoja kukua na serikali kwa ujumla,wananchi watasafirisha mazao kwa urahisi,akina mama watawahi hospitalini wakati wa kujifungua na hivyo kupunguza vifo vya mama na mtoto,"alisema.
Aidha amesema Rais Samia ameongeza kiasi Cha Bilioni 125 Ili kukamilisha ujenzi wa maboma ya Madarasa 10,000 kwa shule ya Msingi na sekondari nchi nzima hatua itakayosaidia kupunguza changamoto za mimba za utotoni na hivyo kumfanya mtoto wa kike atimize ndoto zake za kupata elimu.
"Chama Cha Mapinduzi CCM kupitia Ilani yake ya Uchaguzi 2020-2025,pamoja na mambo mengine imeahidi kuboresha huduma za afya, na Rais Samia ameibeba dhamira hii kwa kutoa nyongeza ya Shilingi Bilioni 100 ili kukamilisha ujenzi wa maboma ya Zahanati nchi nzima,ametoa nyongeza.ya Shilingi Bilioni 100 kwa ajili ya ununuzi wa dawa, vifaa tiba na vitenganishi,"alisema.
Mbali na hayo amesema,kupitia dhamira yake ya kujenga Shule za sayansi kwa wasichana nchi nzima anaenda kumkomboa msichana kwa kuongeza idadi ya Wasichana wataalamu kwenye masomo ya Sayansi nchini.
Mtaturu amesema hayo ni kwa uchache Kati ya mengi yenye maslahi kwa Taifa yaliyofanyika.
Kutokana na hayo amemfananisha Rais Samia na mwamba ulio imara, mwanamke shupavu,jasiri,ambaye tangu Machi 19,2021 aandike historia ya kuwa Rais wa kwanza mwanamke amedhihirisha kiu yake ya kuhakikisha kila alipangalo linafanikiwa.
Akizungumzia kuhusu yaliyofanyika jimboni,Mtaturu amesema jumla ya Milioni 700 zimeelekezwa kujenga vyumba vya madarasa kwenye shule za msingi na Sekondari .
"Sio hilo tu maabara za kujifunzia masomo ya sayansi kwenye shule za Sekondari zimejengwa,"aliongeza.
Amesema Rais Samia amebeba dhamira ya kumtua mama ndoo ya maji kichwani ambapo ameelekeza Shilingi Bilioni 1.7 kwenye miradi ya Maji.