Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 5:09 pm

NEWS: SERIKALI YAJIPANGA KUPATA SAMPULI ZAIDI YA 100000.

DODOMA: Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya amesema Wizara yake imepanga kupata sampuli zaidI 100,000 kuanzia kitongoji hadi Kata ili kuwasaidia wakulima kulima mazao kulingana na udongo wa sehemu aliopo.


Akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wakihuisha mkataba dhidi ya AGRA amesema wameamua kufanya hivyo ili kuwasaidia wakulima waweze kuchangia sekta ya Kilimo kwakuongeza tija na pato la taifa.

Amesema kusaini mkataba ni hatua moja lakini hatua muhimu ni kusimamia kiweledi kuhakikisha wakulima wananufaika lakini pia yaliopo kwenye mkataba yanatekelezwa ipasavyo.

"Wizara itafuatilia kwa karibu utekelezaji wa mkataba pamoja na mikataba mingine iliosainiwa na wizara, "amesema Kusaya.

Ameendelea kwa kusema wizara itaendelea kushirikiana na taasisi hii katika maeneo makuu yafuatayo ili kuimarisha ujuzi wa biashara kwa wakulima wadogo.

Alisema katika pia watatoa msaada wa kifedha kwa ajili ya maendeleo ya Kilimo kwa kujenga uwezo wa kitaaluma na kupanga mipangp pamoja kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika sekta ya Kilimo.

Amesema wizara itaendelea kuimarisha mahusiano pande zote mbili kwa kuwepo kwa ofisi ya uratibu kwa ajili ya kuratibu kazi za AGRA ikiwemo kuendeleza tathmini ya pamoja kati ya pamoja ili kuendelea kubaini kiwango cha utekelezaji.

Akizungumzia kuhusiana sampuli za udongo, amesema wamejipanga kuhakikisha zoezi hilo litafanyika kuanzia ngazi yavitongoji hadi juu..

Awali Mwakilishi wa AGRA-ALLIANCE Afrika Vianey Rweyendela amesema utiaji saini mkataba kuhuisha makubaliano kati ya wizara na AGRA ni jambo zuri kwa sababu litsaidia kuboresha sekta ya Kilimo.

Rweuendela alisema anawashkuru wizara ya Kilimo kwa kuendelea kufanya kazi pamoja ambayo inaonyesha mafanikio makubwa katika sekta ya Kilimo lakini pia kuwanufaisha wakulima wadogo kwa wakubwa.

Amesema wataendelea kuandaa miradi mbalimbali kwa pamoja ili kuhakikisha sekta hiyo inasonga mbele.

Hata hivyo alisema wizara iko mstari wa mbele kuhakikisha wanafika mbele katika sekta ya Kilimo.