Home | Terms & Conditions | Help

Tue Apr 08 2025 12:25:23 PM

NEWS: SEREKALI YAIFUNGIA TIMU YA JKT TANZANIA KUINGIA NA MASHABIKI

Serikali imetangaza kuifungia timu ya JKT Tanzania kucheza wakiwa na mashabiki kwenye michezo yake iliyosalia katika uwanja wa nyumbani wa Jamhuri jijini Dodoma.

Uamuzi huo wa Serekali umetolewa baada ya mashabiki wa club hiyo kujazana na kushindwa kufuata tararibu za wizara ya afya kwenye mchezo wake wa jana wa dhidi ya Yanga.

Serekali imesema kuwa Timu hiyo ilikiuka kanuni ya 2.0.2(iii) inayosisitiza kukaa mita moja moja baina ya mtu na mtu.

Kwa mujibu wa taarifa ya Serikali kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Lorietha Lawrence, mashabiki walijazana sana uwanjani hivyo kukiuka kanuni inayoagiza kufuatwa muongozo wa umbali wa mita moja kutoka shabiki mmoja na mwingine.

Aidha taarifa hivyo imesisitiza vilabu wenyeji, wasimamizi wa michezo na wadau wengine kuendelea kusimamia kikamilifu muongozo wa Afya na taratibu nyingine ili kujikinga na maambukizi ya Covid-19.