- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RC MTAKA ATANGAZA SIKU 10 KUJUA MBIVU NA MBICHI WAMILIKI WA ARDHI.
DODOMA; Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma imetenga siku kumi (10) kwaajili ya kushughulikia migogoro ya Ardhi kwenye kata 41 na mitaa 226 ya jiji la Dodoma.
Zoezi hilo litashirikisha watalaamu wa Ardhi kutoka Wizara ya Ardhi ,Ofisi ya Ardhi ya Mkoa ,Ofisi ya jiji la Dodoma na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Ofisini kwake,Mkuu wa Mkoa huo Anthony Mtaka, amesema imeundwa timu ambayo itahusisha watu wote ikiwemo Maafisa Ardhi,Maafisa Mipango,Wanasheria,Afisa wa utoaji hati,Ofisi ya Baraza la Ardhi na Maafisa ambao uwepo wao kwenye timu hiyo watatoa majawabu ya moja kwa moja kwa wananchi ambao watawafikia.
Aidha,Mtaka amesema zoezi hilo litaendeshwa kwa njia ya teknolojia ikiwa mwananchi anayehudumiwa kuazia Julai 5 hata kama viongozi aliyowakuta kwa siku ya kwanza hawapo atakapo kwenda kwenye Ofisi ya Serikali kuhusu suala la ardhi atashughulikiwa vizuri.
Wakati huo huo ,Mtaka amewataka Wananchi wa Dodoma kutumia fursa hiyo ya siku kumi (10) ili kupunguza shida za wanachi kutoka nyumbani kwenda ofisini kwake kwaajili ya kushughulikiwa migogoro hiyo.
Katika hatua nyingine ,Mtaka amesema zoezi hilo litakapomalizika katika jiji la Dodoma litaenda katika Wilaya zilizopo Mkoani humo.
Hata hivyo,Mkuu huyo wa Mkoa ameendelea kuwasisitiza wanachi kuwa kila mwenye mgogoro wa Ardhi aende kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete ili Maafisa wanapokwenda kule wawakute.