Home | Terms & Conditions | Help

November 21, 2024, 3:36 pm

NEWS: RAIS MWINYI AMTUMBUA KATIBU WA RAIS ALIYEMTEUA MWEZI MMOJA

Dar es Salaam. Taarifa kutoka ikulu ya Zanzibar imeripoti kuwa Rais mpya wa sasa wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi ametengua uteuzi wa katibu wa rais, Suleiman Ahmed Saleh ikiwa ni mwezi mmoja tu tangu alipomteua kuwa Katibu wake wa Ikulu.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu Desemba 14, 2020 na katibu mkuu kiongozi, Dk Abdulhamid Mzee inaeleza kuwa rais Mwinyi amechukua hatua hiyo kutokana na uwezo alionao kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar.

“Chini ya kifungu cha Na.53 cha Katiba ya Zanzibar ya 1984 na kifungu 12(3) cha Sheria ya Utumishi wa umma Namba 2 ya mwaka 2011, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi ametengua uteuzi wa katibu wa Rais, Suleiman Ahmed Saleh,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo ikibainisha kuwa atapangia kwazi nyingine.

Dk Mwinyi alimwapisha Ahmed Novemba 7, 2020 katika hafla iliyofanyika Ikulu mjini Unguja na hakuna taarifa ya ziada inayoelezea sababu za Rais Mwinyi Kumtoa katika nafasi hiyo aliyodumu nayo kwa kipindi cha mwizi mmoja.

Rais Mwinyi tangu kuingia Ikulu amekuwa na kibarua cha kuteua watu mbalimbali katika nafasi mbali mbali ili kuweka sawa safu yake ya kufanya kazi kwa kipindi cha miaka 5 ijayo.

Hivi karibuni Mwinyi ameteua viongozi waandamizi wa chama kikuu cha Upinzani visiwani Zanzibar cha ACT Wazalendo kuwa wabunge wa Baraza la wawakilishi katika bunge la Zanzibar.

Wabunge walioteuliwa ni Makamu mwenyekiti wa ACT Wazalendo Zanzibar Nassor Mazrui na Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho Saidi Omari Saidi.