- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIA WA BURUNDI WANAPIGA KURA LEO
Wananchi wa Burundi leo Jumatano mei 20, 2020 wanapiga kura kumchagua rais na wawakilishi wengine kama wabunge katika Uchaguzi unaofanyika licha ya Dunia na nchi hiyo kukabiliwa na janga la Corona.
Huu ni uchaguzi ambao unawakutanisha wagombea saba wanaotafuta urais, kuchukua nafasi ya rais Pierre Nkurunziza ambaye hawanii tena baada ya kuwa madarakani kwa miaka 15.
Wachambuzi wa siasa wanasema ushindani mkali unatarajiwa kuwa kati ya mgombea wa chama tawala CNDD-FDD Jenerali Evariste Ndayishimiye, na kiongozi wa zamani wa waasi Agathon Rwasa, kutoka chama kikuu cha Upinzani CNL.
Tume ya Uchaguzi nchini humo imesema wapiga kura zaidi ya Milioni TANO, wanatarajiwa kushiriki katika uchaguzi huu ambao utapelekea kubadilishana kwa madaraka kwa amani kwa mara ya kwanza tangu nchi hiyo ya Afrika ya Kati ipate uhuru mwaka 1962.
Kuelekea Uchaguzi huu, kumeshuhudiwa makabilianio kati ya wafuasi wa chama tawala na wale wa chama kikuu cha upinzani, huku kila upande ukilaumiana.
Uchaguzi huu hautakuwa na waangalizi wa kimataifa na wale wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotarajiwa kuwasili nchini humo, walitangaziwa kuwekwa karatini kwa siku 14 kutokana na janga la Corona na hivyo kuwaondoa katika zoezi hilo, hatua ambayo imewanfanya wachambuzi wa siasa kuhoji iwapo zoewi hilo litakuwa huru na haki.
Vituo vya kupigia vimefunguliwa saa 12 asubuhi saa za Afrika ya Kati na kufungwa saa 10 jioni, huku matokeo ya mwisho yakitarajiwa kutangazwa mapema mwezi Juni.