Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 6:57 pm

NEWS: NYALANDU ACHUKUA FUMU YA KUWANIA KUGOMBEA URAIS

Aliyewahi kuwa waziri wa Maliasili na Utalii nchini Tanzania Lazaro Nyalandu amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea urais kwa tiketi ya chama cha Upinzani Chadema.

Nyalandu ambaye alikuwa Mbunge wa Singida Magharibi amesema leo Julai 8, 2020 kuwa endapo atapata ridhaa ya kuwa Rais wa Tanzania atahakikisha analirudisha taifa katika umoja wa kitaifa.

"Nilipokuwa CCM tukimaliza uchaguzi tulikuwa tunapiga wimbo 'Wacha waisome namba', sasa sisi hatutaki Mtanzania yoyote aisome namba. Naitamani Tanzania ambayo mpinzani ana fursa kamili kuwakosoa watawala" - Lazaro Nyalandu

"Saa imefika tuwaambie Watanzania kuwa yale wanayoyatamani kuyaona, wanayotamani kuwa nayo yanawezekana. Wale wanaowaombea wenzao kutofanikiwa hawatosimama"

"Hizi habari za kwamba mtu amekutwa na kosa halafu anakaa Keko kizuizini mwaka wa kwanza na wa pili na wa tatu zitakuwa ni historia. Hatutawaweka watu kizuizini awe CHADEMA au CCM"

"Wakati najivua ujumbe wa Halmashauri Kuu CCM nilisema ili nchi iende sawasawa ni lazima Bunge liwe huru, kuwe na nchi ambayo mwananchi akikosewa ataipeleka Serikali yake mahakamani"

"Tuione nchi iliyo yenye amani, nchi ambayo watoto wake wataiona heri. Naitamani Tanzania ambayo tofauti yako ya kisiasa haitakuwa njia ya kutugawa, kuanzia mwana CHADEMA, CCM, NCCR-mageuzi, ACT wazalendo watatembea kifua mbele" - amesema Nyalandu