- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS; MTATURU AMPA TANO RAIS SAMIA.
DODOMA; Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu amesema bajeti kuu ya Serikali 2021/2022 iliyowasilishwa Juni 10 bungeni,imebeba kauli mbiu ya Kazi Iendelee kwa vitendo.
Akichangia bajeti hiyo Juni 17 bungeni,Mtaturu ameipongeza serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa bajeti nzuri inayomgusa mwananchi na iliyosikiliza kilio cha wabunge.
“Nampongeza Rais wetu,Jemedari wetu kwa kuendelea kuongoza vizuri nchi yetu na kwa namna ambavyo amekuwa akisikiliza maoni ya wabunge,miongoni mwa sifa inayompamba kiongozi ni kusikiliza watu wake,mama yetu anatusikiliza na anawasikiliza wananchi na anatuongoza vizuri,tunampongeza na kumtakia afya njema,
“Rais Samia amenyesha dhahiri kuwa hii ni bajeti ya kazi iendelee kwa sababu miradi yote ya kimkakati amesema itaendelea na juzi akiwa Mwanza amezindua tena ujenzi wa Reli ya SGR kutoka Mwanza hadi Isaka maana yake itakutana katikati iweze kukamilika ianze kufanya kazi,”alisema.
Amesema pongezi hizo zinatokana pia namna bajeti ilivyogusa maeneo yote muhimu hususan katika sekta ya miunddombinu ambapo kwenye barabara hasa za vijijini fedha zimetolewa kwa kila jimbo kiasi cha Shilingi Milioni 500.
OMBI LA UJENZI WA SOKO NA STENDI.
Ili kuongeza mapato katika Halmashauri na serikali kwa kuu,ameomba kuanza kwa utekelezaji wa mradi wa kimkakati wa Soko na Kituo cha Mabasi.
“Wilaya ya Ikungi tulikuwa na maombi ya muda mrefu ya kuwa na kituo cha mabasi maana hatuna inayoweza kukidhi haja iliyopo katika wilaya yetu,pia tupate soko la kisasa ili kuongeza mapato ya halmashauri na hivyo kusaidia bajeti ya serikali kwenye kuleta maendeleo ya nchi yetu katika vijiji na halmashauri zetu,”aliomba.