- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MTATURU ALIA NA WASTAAFU WALIPWE MAFAO MAPEMA
DODOMA: Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameiomba serikali kuwalipa mapema wastaafu mafao yao ambao wamelitumikia Taifa hili kwa uadilifu.
Akichangia mjadala wa bajeti ya wizara ya fedha na mipango kwa mwaka 2020/2021 Mtaturu amesema kuna baadhi ya Wastaafu wamekuwa wakicheleweshewa mafao yao.
“Katika wilaya ya Ikungi kuna wazee wawili Mohammed Ntandu na Gamiliel Massawe wanalalamika hawajatendewa haki huu mwezi wa Saba Sasa,wakienda NSSF hawawapi majibu mazuri naomba mh waziri kuwe na connection nzuri kati ya mikoa na hazina ili kuwasaidia wastaafu wapate mafao yao mapema,”alisema Mtaturu.
Mbali na hilo ameiomba Wizara itoe fedha kwa ajili ya mradi wa umwagiliaji wa Mang’onyi Kata ya Makiungu kwa kuwa mradi huo una faida nyingi kwa wananchi,lakini kwa halmashauri pia.
“Kuna mradi wa skimu ya umwagiliaji ya Mang’onyi,hiyo skimu ilitengewa fedha mwaka 2017/2018 ilitengewa shilingi milioni 100 lakini fedha zile hazikwenda leo hii lile bwawa kina chake kimepungua hivyo hatuwezi kuwa na maji ya kutosha na mwaka huu mvua zilivyokuwa nyingi lile bwawa lilitapika na kutaka kuleta athari kwa wananchi.
“Naomba fedha tunazoomba tuwe tunapewa ili tuweze kuboresha ile skimu ambayo ipo pale itaenda kunufaisha wakulima wengi,”alisema.
Aidha amewaomba watanzania kuhakikisha katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu wanachagua CCM chama ambacho ndicho kitakachowaletea maendeleo.
“Unapokuwa na aina ya vyama vya siasa ni lazima uwe na vyama vyenye focus ya kuwatumikia wananchi,na mnaona wenyewe watanzania wameona vyama hivi kuna baadhi ya vyama tukikutana octoba kitatoka kuwa chama cha siasa kitakuwa ni kikudi cha watu wawili watatu.
“Nimtie moyo Rais kwa kazi kubwa anayoifanya kwa hakika watanzania wamemuelewa watanzania hawatamuacha haya yote makubwa aliyoyafanya hayatafutika katika uso wa watanzania,nimtakie kila la kheri,sisi wapiganaji tupo pamoja nay eye na kwa Singida Mashariki nimuhakikishie kura nyingi,mbunge nipo na madiwani wote watapatikana na CCM,”alisisitiza Mtaturu.
Akijibu hoja zilizotolewa wakati wa mjadala waziri wa fedha na mipango dkt Philip Mpango amesema moja ya kipaumbele chake ni kuhakikisha wazee wanastaafu kwa amani kwa kuwalipa mafao yao kadri inavyostahili.
Amesema kwa sasa serikali wanajitahidi kadri inavyowezekana kuhakikisha wazee wanaostahili mafao wanayapata kwa wakati.
“Nimepokea kilichosemwa na mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu,na bahati nzuri ameniwasilishia document hivyo nitazifuatilia,kinachotusumbua mara nyingi ni udhaifu katika taarifa lakini katika wizara tumeweka kipaumbele chetu ambacho ni kuhakikisha wazee wetu wanastaafu kwa amani kabisa,”alisema Dkt Mpango.