- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: Mtaturu aibana serikali kwenye elimu.
DODOMA: Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameihoji serikali ni lini itajenga Shule ya Sekondari ya Kidato cha Tano na Sita katika Kata ya Mungaa ambayo ni ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoitoa kipindi cha Kampeni 2020.
Akiuliza swali Septemba 9 Bungeni Jijini Dodoma,Mtaturu amesema ujenzi wa shule hiyo ni ahadi ya Rais Samia aliyoitoa alipopita kwenye jimbo hilo.
Akijibu swali hilo,Naibu Waziri Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),David SIlinde amesema serikali imejipanga kujenga shule za sekondari za wasichana kila Mkoa na nyingine 1,000 kwa kata zisizo na shule hizo ili kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani na vikwazo hususani watoto wa kike kutembea umbali mrefu.
Amesema Shule 26 za wasichana zitajengwa kwa awamu kwa kila Mkoa na kwamba watafanya upanuzi wa Shule za sekondari 100 ili kupokea wanafunzi zaidi wa kidato cha tano na sita.
Amefafanua kuwa awamu ya kwanza ya ujenzi itaanza mwaka wa fedha 2021/2022 ambapo serikali imetenga jumla ya Shilingi Bilioni 220.
Aidha,imesema kabla ya kuanza kwa ujenzi huo itafanya tathimini ya maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule za Sekondari mpya na mahitaji ya upanuzi wa Sekondari za kidato cha tano na sita ikiwa ni pamoja na Shule ya Sekondari Mungaa.
Katika swali la nyongeza mbunge huyo ameomba tathimini hiyo itakayofanyika ichukue umuhimu wa pekee kuhakikisha shule ya Mungaa ambayo ni kongwe inajengwa .
“Katika vikwazo mojawapo alivyoeleza ni pamoja na vikwazo kwa watoto wa kike katika shule zetu za sekondari ikiwemo shule za kata,sasa nini mkakati wa serikali kujenga hostel za kuweza kuchukua wanafunzi wote wa kike katika shule zetu ambazo zipo kwenye jimbo la Singida Mashariki.
Akijibu swali hilo Silinde amesema katika tathimini ya shule 100 wanazoenda kuzifanyia upanuzi nchi nzima ili kupokea watoto wa kidato cha tano,miongoni mwa shule itakayofanyiwa tathimini ni shule ya Mungaa.
“Moja ya mkakati wa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ni pamoja na kujenga hostel ndio maana mwaka huu wa fedha tumetenga fedha nyingi katika kuhakikisha kwamba tunajenga hostel katika maeneo mbalimbali,nyinyi mmepitisha bajeti tunasubiri fedha zitakapotoka tutaainisha maeneo mbalimbali na tutazingatia Maeneo ya Singida Mashariki .