March 15, 2025, 6:19 am
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MKUU WA MAJESHI AWAONYA WANAJESHI KUJIHUSISHA NA SIASA
Mkuu wa Majeshi nchini Tanzania Jenerali Jacob Mkunda amewataka wanajeshi wote nchini wakiwemo Wahitimu wapya wa Jeshi hilo kutojihusisha kabisa na siasa wakati wote watakapokuwa wakilitumikia Jeshi hilo.
Jenerali Mkunda ameyasema hayo hii leo Jumamosi Octoba 1, 2022 katika kikosi cha 833 KJ Oljoro Wilayani Arumeru wakati akifunga mafunzo ya Kuruta 41/22 yaliyowashirikisha Askari 2457 huku 80 kati yao wakishindwa kumaliza mafunzo hayo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utovu wa nidhamu na vifo.
Vilevile Jenerali Mkunda amekemea tabia ya Wanajeshi kupigana wenyewe kwa wenyewe na kusema ikibainika ni wote watafukuzwa jeshini mara moja
Newest Posts