Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 5:10 am

NEWS: MEYA ALIYEPIGA MARUFUKU UVAAJI BARAKOA AELEZA SABABU NYINGINE

Moshi. Mara baada ya kikao Meya wa manispaa ya Moshi, Juma Raibu alifafanua kuwa aliwataka wajumbe waliokuwa wamevaa barakoa katika kikao cha bajeti cha baraza la madiwani manispaa hiyo kuzivua kwa sababu uvaaji huo huongeza hofu ya ugonjwa wa corona kwa wananchi.

Ameeleza hayo jana Alhamisi Januari 28, 2021 baada ya kumalizika kwa kikao cha kupitisha bajeti ya manispaa hiyo, akibainisha kuwa pamoja na kutakiwa kuchukua tahadhari haitakiwi kupeana hofu

"Nimeona katika baraza madiwani karibu thelathini, wapo viongozi wa serikali na viongozi wa vyama walioalikwa wote hawa hawajavaa barakoa hata mmoja, lakini limekuja kundi la watu wamevaa barakoa jambo ambalo wanaamini halmashauri hii ina corona.”

"Nimewaambia wavue waendelee kuamini kuwa corona ipo na tujiendelee kujikinga lakini manispaa ya Moshi haina corona, tuendelee kujikinga katika mambo mengine ila tusitiane hofu, katika baraza langu la manispaa sitaruhusu mtu yeyote kuingia na barakoa katika kikao changu kwani ninaamini tuko salama,” amesema