- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MCHEKESHAJI IDRIS SULTAN AKAMATWA NA POLISI
Dar es salaam. Msaanii wa vichekesho nchini Tanzania Idris Sultan anashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam kwa makosa ya kimtandao.
Idris (27) anashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay Jijini Dar es salaam na ni baada ya kuwasili hapo mchana wa leo kufuatia wito wa Polisi.
Mwanasheria wake amesema anahojiwa kwa “Makosa ya Mtandao”
Imedaiwa atahamishiwa Makao Makuu ya Polisi
Kama utakumbuka mwezi Oktoba 2019, mchekeshaji huyo alikamatwa kwa kuhariri picha ya Rais Magufuli na alihojiwa kwa saa 5 katika Kituo cha Polisi Central, kisha kuachiwa kwa dhamana
Aidha, Idris aliyewahi kushinda tuzo ya Big Brother Africa mwaka 2014, Machi mwaka huu alifikishwa katika Mahakama ya Kisutu kwa kuweka maudhui mtandaoni bila leseni.