Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 3:26 am

NEWS: MBARONI KWA WIZI WA TAIRI ZA GARI LA KAMANDA WA POLISI GEITA

Jeshi la polisi mkoani Geita linawashikilia majambazi wawili kwa tuhuma za kuvamia gari la kamanda wa polisi mkoa huo na kuiba matairi yake yote manne kisha kutokomea pasipojulikana.

WAWILI WAUAWA KISHA KUNYOFOLEWA VIUNGO VYAO | MALUNDE 1 BLOG

Wezi hao walivamia usiku wa manane kwa kushirikiana na walinzi wa eneo hilo lililokuwa limehifadhiwa gari la kamanda wa polisi mkoa huo na kufungua matairi yote na kisha kutokomea nayo kusiko julikana .

Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Mponjoli Lotson anasema katika hali isiyo ya kawaida watu hao kwa kushirikiana na walinzi walifanya uporaji huo kwa kufungua matairi hayo kisha kutokomea nayo huku jeshi hilo likiendelea na msako ili wahusika wote wakamatwe na kuchukuliwa hatua.

Aidha Kamanda Lotson amesema Jeshi hilo naendelea kuwasaka watu wengine kadhaa waliohusika na Uhalifu huo.