Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 1:21 am

NEWS: MAHAKAMA YAIPA SEREKALI MIEZI 18 KUREKEBISHA KIFUNGU CHA KUMNYIMA ZAMANA MTUHUMIWA

Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es salaam imeamuru kuwa kifungu Cha 148(5) Cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai kinachomnyima mtuhumiwa dhamana kufanyiwa marekebisho ndani ya MIEZI 18 kwasababu kinakiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mahakama hiyo imefikia uamuzi huo leo Mei 18, 2020 Wakati ikitoa Hukumu juu ya Kesi ya Wakili Dickson Sanga dhidi ya mwanasheria Mkuu wa serikali akipinga Watuhumiwa nchini kunyimwa dhamana chini ya Kifungu Cha 148(5) Cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai.

Kifungu hiki cha sheria kimewahi kukoselewa kwenye kesi ya DPP dhidi ua Daudi Pete ambayo Mahakama ilitoa uamuzi kwamba kifungu hicho ni null and void kwasababu kinakiuka kifungu 13(6) cha katiba ya Muungano wa Tanzania na Mahakama imetoa wiki 18 tu kwa kifungu hicho kibadilishwa.