Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 1:22 am

NEWS: MAHAKAMA KUTOA HUKUMU MAPINGAMIZI YA MBOWE

Kesi namba 21/2021 iliyofunguliwa katika Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es salaam na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP)na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) imehairisha hii leo Agosti 30, 2021 mpaka Septemba 23 mwaka huu.

Mahakama Kuu hiyo inatarajia kutoa uamuzi tarehe hiyo ya Septemba 23, 2021 juu ya mapingamizi manne yaliyowasilishwa na upande wa Jamhuri.

Mapingamizi hayo ya serikali kwenye kesi hiyo iliyopo mbele ya Jaji John Mgeta, ni kutaka kesi hiyo iliyofunguliwa na Mbowe iondolewe mahakamani hapo kwa madai ya kuwa utaratibu uliotumika kufungua kesi hiyo umekiuka sheria.

Upande wa Jamhuri umeiomba mahakama kusikiliza mapingamizi hayo yaliyowasilishwa ma Wakili wa Serikali Mkuu, Hangi Chang'e huku kusikilizwa kwa njia ya maaandishi.

Upande wa utetezi katika kesi hiyo unawakilishwa na Jopo la Mawakili Saba, wakiongozwa na Peter Kibatala ambao wamesema hawana pingamizi na hoja za Serikali utaka kusilizwa kwa njia ya maandishi mbele ya Jaji Mgeta.

Baada ya serikali kutoa hoja hiyo, Jaji Mgeta akatoa utaratibu wa namna pande zote mbili zitawasilisha hoja zao ambapo Pande zote zimekubaliana kuwasilisha hoja zao kuanzia Septemba 6, 9 na 13, 2021. ambapo Septemba 23 saa nane mchana Jaji Mgeta atatia uamuzi.