- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MADEREVA 23 KUTOKA TANZANIA WAKUTWA NA CORONA KENYA
Madereva 25 kutoka nchini Tanzania wamezuiwa kuingia nchini Kenya baada ya kupimwa na kungudulika kuwa na Virusi vya corona.
Kati ya madereva hao 23 ni raia wa Tanzania , mmoja wa Uganda na mmoja kutoka taifa la Rwanda.
Kulingana na wizara ya afya nchini Kenya raia hao wa taifa jirani la Tanzania walipimwa na kupatiwa matokeo yao katika kipindi cha saa 24.
Wizara hiyo imesema kwamba hatua hiyo inalenga kuwalinda Wakenya dhidi ya maambukizi kutoka kwa raia wa kigeni.
Katika mkutano wake na wanahabari naibu waziri wa Afya rashid Aman amesema kwamba maabara 2 za kuhama hama zitazinduliwa katika mpaka wa Namanga ili kuimarisha upimaji wa wagonjwa wapya.
Aman aidha amewataka Wakenya wanaoishi mipakani kuwaripoti watu wanaowashuku ambao wanajaribu kuingia nchini kwa njia haramu.