Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 4:15 am

NEWS: KESI YA GODBLESS LEMA YAPIGWA KALENDA

Kesi inayomkabili Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema kupitia chama Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), imeahirishwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida hadi June 11 mwaka huu baada ya upande wa Jamhuri kuileza Mahakama kuwa upelelezi bado haujakamilika.

Mbunge Lema anakabiliwa na mashtaka 15 iliwemo la kusababisha taharuki kwa jamii baada ya kusambaza taarifa zinazodaiwa za upotoshaji kuhusu mauaji ya watu 14 wilayani Manyoni mkoani Singida.

Mshakiwa Lema anadaiwa kutenda makosa hayo 15, Februari 29 mwaka huu wilayani Manyoni.