- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KENYATTA AAHIDI KUMUHARIBIA RUTO KWENYE URAIS
RAIS wa Kenya Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto wametishiana kupakana matope hadharani huku siasa za kuchafuliana majina zikionekana kushika kasi nchini Kenya.
Kulingana na viongozi wa Jubilee, Rais Kenyatta anajiandaa kuzuru eneo la Mlima Kenya ambapo wandani wake wanasema atafichua “maovu ya naibu wake” na kuwaelezea wakazi kiini cha kutengana kwao.
Kwa mujibu wa Mbunge wa Nyeri Mjini, Wambugu Ngunjiri, Rais Kenyatta anatarajiwa kufichua siri ‘nzito’ ya Dkt Ruto kuhususu “maovu aliyotenda” tangu walipochukua hatamu za uongozi 2013.
Mabwanyenye wa Mlima Kenya walipoidhinisha rasmi kuunga mkono kinara wa Azimio la Umoja, Raila Odinga mnamo Disemba mwaka jana, pia walitishia kufichua men – gi kuhusu Ruto.
Mnamo Ijumaa wiki iliyopita, Rais Kenyatta alirusha tope la kwanza kwa naibu wake alipodai Dkt Ruto alikuwa waziri wa kilimo wakati viwanda vya sukari katika eneo la magharibi mwa Kenya vilipoporomoka.
“Leo ninazomewa kuhusu kuporomoka kwa viwanda vya sukari vya Mumias na Nzoia. Wakati viwanda hivyo viliporomoka, mimi sikuwa rais. Yeye (Ruto) ndiye alikuwa waziri wa kilimo,” Rais Kenyatta akaambia kundi la vijana waliokongamana katika Ikulu ya Nairobi.