- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KENYA YAFUNGA MIPAKA YAKE NA TANZANIA
Serekali ya Kenya imeamua kufunga mipaka yake ya Kimataifa ya Tanzania na Somalia kwa muda wa siku 30 kuanzia saa sita usiku ya leo Jumamosi Mei 16, 2020.
Katika hotuba yake kwa taifa Rais Uhuru Kenyatta amesema hatua hiyo inajumuisha udhibiti usafiri wa watu kutoka mataifa hayo kuingia nchini Kenya.
Hatahivyo usafirishaji wa mizigo utaindelea kati ya Kenya na mataifa hayo mawili.
Marufuku hiyo ya kuzuia watu kutoka Tanzania na kuingia nchini Kenya inaanza usiku wa leo saa 6 na kuruhusu mizigo tu kupita.
Na kwa upande wa Somalia masharti ni hayo hayo, mizigo peke yake ndio itaruhusiwa.
Aidha madereva watakaoingia nchini Kenya kuleta mizigo watatakiwa kupima corona kwanza.
Kenya imeongeza tena muda wa marufuku ya kutoka nje kwa muda wa siku 21.
Kufikia sasa idadi ya watu walioambukizwa na virusi vya corona nchini Kenya imeongezeka hadi 830 baada wagonjwa wapya 49 kuthibitishwa kuwa na ugonjwa huo.
Waliofariki kutokana na corona ni watu 50 baada ya wengine watano kufa.
Rais Kenyata pia ametangaza kuwa wagonjwa 17 wametolewa hospitalini walipokuwa wakipata matibabu.
Rais Kenyatta pia ameongeza muda wa watu kutoka nje wa kuanzia saa moja usiku hadi saa kumi na moja asubuhi hadi Juni 6,2020.
''Najua Wengi wanataka maisha yarudi kama vile ilikuwa lakini wenzagu sitaki niwadanganye. Jukumu la kwanza la serikali ni kulinda maisha ya Wakenya'', alisema.
Marufuku ya usafiri kuingia na kutoka miji mitano ikiwemo Nairobi, pia imeongezwa kwa siku 21.