Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 1:58 am

NEWS: KAULI YA DKT NDUGULILE BAADA YA KUFUTWA KAZI

Aliyekuwa Naibu waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile amemshukuru Rais Magufuli kwa Kumuamini kwa kipindi chote hicho akiwa kama Naimbu Waziri wa Afya.

Kauli hii ya Dkt Ndugulile inakuja siku moja mara baada ya Rais Magufuli Kutengua uteuzi wake kama Naibu Waziri.

Ndugulile amesema kuwa amepokea uamuzi wa Mhe Rais kwa unyenyekevu mkubwa. "Ninamshukuru sana Mhe Rais kwa imani yake kwangu na kwa kunipa fursa ya kuhudumu katika Serikali yake" amesema Ndugulile.

"Nawashukuru sana Ummy Mwalimu, watendaji na watumishi wote katika sekta ya Afya kwa ushirikiano walionipatia.

"Mafanikio ya sekta ni makubwa sana na ni ya kujivunia. Nafarijika kuwa sehemu ya mafanikio haya. Tuendelee kuongeza bidii kufikia malengo makubwa zaidi.

Namtakia kila la kheri Naibu Waziri ajaye Dkt Mollel na nitampatia ushirikiano wote" amesema Dkt Ndugulile