Home | Terms & Conditions | Help

Wed Apr 09 2025 2:02:17 PM

NEWS: CUF YAWAJIBU WABUNGE WALIOHAMIA ACT

Dar es salaam. Chama cha wanchi CUF Kimesema kuwa Wabunge waliohamia chama cha ACTwazalendo hii leo walishaamua kujitenga na chama cha CUF tangu mwezi March 2019 na hawajawahi kutoa Ushirikiano kwa CUF tangu muda huo.

"CUF iliamua kutowafukuza ili kudhibiti matumizi mabaya ya Kodi za Wananchi kwa ajili ya Chaguzi ndogo" imesema taarifa ya Chama hicho Jioni ya Leo Juni 20, 2020.

Kauli hiyo ya CUF imetolewa saa chache mara baada ya Mkutano wa Leo wa Viongozi waaandamizi wa chama cha Act Wazalendo kuwatambulisha na kuwapatia kadi zao wabunge 21 waliokuwa wakihuduma kupitia chama cha CUF.

Hafla ya kuwakaribisha wabunge hao na madiwani 9 ilifanyika hii leo katika Hoteli ya Lamada iliyopo Jijini Dar es salaam.

Mkutano huo ulikuwa na viongozi wawili, Mwenyekiti wa chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad na Kiongozi Mkuu wa chama hicho Zitto Kabwe waliokuwa wakiwakaribisha wanachama hao wapya wa chama hicho kutoka CUF.

CUF imesema kuwa haikuchukua hatua ya kuwafukuza wabunge hao baada ya kutoonesha ushirikiano na Chama kwa maslahi mapama ya nchi ili kuepusha kuiingiza gharama Serekali.