- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BOSS WA IPTL AHUKUMIWA KULIPA BILIONI 26
Dar es salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam imemuhukumu Mmiliki wa Kampuni ya Kufua umeme ya IPTL, Harbinder Seth kulipa fidia ya Shilingi BILIONI 26 za Kitanzania baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Hukumu hiyo ya Seth imetolewa ikiwa ni utekelezaji wa sheria ya ‘Plea Bargain’ aliyofanya na DPP, Sylveter Mwakitalu, ya kumaliza kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa ikimkabili.
Hukumu imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi leo June 16, 2021 ambapo amesema.
“Ni dhahiri umekaa mahabusu kwa muda mrefu takribani miaka minne ni muda mwingi wa kutosha na ni wazi umeona mengi na kujifunza mengi ukiwa gerezani”
"Pia kwa mantiki hiyo Mahakama inaamua kukupa onyo usije ukatenda makosa tena na utakuwa chini ya uangalizi kwa muda wa mwaka mmoja hayo ndio maamuzi ya Mahakama, kuhusu nyaraka mbalimbali ikiwemo Passport ya kusafiria arudishiwe” Hakimu Huruma Shaidi.