Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 3:47 pm

NEWS: BENKI KUU YAICHUKUA BENKI YA CHINA COMMERCIAL BANK

Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imechukua usimamizi wa China Commercial Bank Limited na kusimamisha Bodi ya Wakurugenzi na uongozi wa benki hiyo ya China hapa nchini baada ya kubaini mapungufu makubwa hasa mapungufu ya mtaji ambayo ni kinyume na matakwa ya sheria ya mabenki na taasisi za fedha nchini.

Uamuzi huo umetangazwa hii leo jijini Dodoma na Gavana wa Benki Kuu Profesa Florens Luoga katika mkutano wake na waandishi wa habari.

Profesa Luoga amesema shughuli za utoaji wa huduma kwa wateja wa China Commercial Bank Limited zinasimama kuanzia leo kwa kipindi cha siku Tisini ili kuipa nafasi BOT kutathmini hatua za kuchukua na kupata ufumbuzi.