Home | Terms & Conditions | Help

Tue Apr 08 2025 1:58:27 PM

MAKONDA: NAUNGA MKONO POLISI KUCHUNGUZWA.

Dar es salaam. Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amesema anaunga mkono hoja ya kamati kuu ya Halimashauri kuu ya chama cha Mapinduzi CCM, ya kuchunguza mwenendo wa baadhi ya maafisa wa jeshi la polisi ambao amewataja kwamba wanaolipaka tope jeshi hilo kwakuwalinda wafanyabiashara MATAPELI wanaodhulumu mali za watu.

"Naomba tuanze na Dar es salaam na mimi PAUL MAKONDA niko tayari kutoa ushirikianao" amesema Makonda Kupitia Ukurasa wake wa Instagram mchana wa leo Marchi 12, 2022.

Kauli hiyo ya Makonda inakuja siku moja mara baada ya kuzuka kwa mgogora baina yake na Mfanyabiashara maarufu nchini Gharib Saidi Mohamed Maarufu kama GSM wakigombania umiliki wa kiwanja no. 60 kilochopo Regent estate manspaa ya kinondoni Dar ea salaam.

Taarifa ya mgogoro huo imekuja siku chache baada ya kusambaa kwa video ambayo Makonda alionekana akidai kuwa eneo hilo ni la kwake huku akiwa amezingirwa na watu akiwemo askari aliyevalia sare za jeshi la polisi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi tarehe 12 Machi 2022, Mwanasheria wa GSM, Alex Mgongolwa, amesema mteja wake amempa maelekezo ya kukanusha umiliki wa Makonda na kuchukua hatua zaidi ikwemo kwenda mahakamani endapo ataendelea kudai eneo hilo ni lake.

“Leo tumewaita hapa ili kuwapa taarifa fupi ya uhalali wa umiliki wa eneo lenye Plot namba 60 lililopo Regent Estate Manispaa ya Kinondoni, Dar Es Salaam,” amesema Mgongolwa.

Mgongolwa amesema Mohammed alinunua ardhi hiyo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya makazi tarehe 21 Novemba 2006 na kuonyesha waandishi wa habari nyaraka za udhibitisho.