- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
IGP SIRRO: POLISI WALIOVUKA MPAKA WA MALAWI WAMETUTIA AIBU
Moshi. Kamanda Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzanoa (IGP), Simon Sirro amesema kitendo cha polisi wake saba waliovuka mpaka wa Tanzania na kuingia nchini Malawi lilikuwa Tukio la aibu sana na kufafanua kuwa mali ya magendo ambayo waliyokuwa wakiyafukuza thamani yake ni Sh30,000.
Mbali na sakata hilo, Sirro amebainisha kuwa kuna changamoto kubwa ya upelelezi inayosababisha mlundikano wa mahabusu na kuwaagiza wanaosimamia madawati ya upelelezi kuhakikisha suala hilo linamalizika.
Sirro ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Oktoba 8, 2021 katika Shule ya Polisi Moshi (MPA) wakati wa mahafali ya kuhitimu mafunzo ya uongozi ngazi ya wakaguzi wasaidizi ambapo maofisa 2,030 walihitimu wengi wakiwa ni wasomi wa vyuo vikuu.
Miongoni mwa waliohitimu mafunzo hayo, mmoja ana shahada ya udaktari wa falsafa, 50 wana shahada ya Uzamivu, 19 wana stashahada ya uzamili na 1,792 wana shahada ya kwanza za chuo kikuu.
Akizungumza katika hafla hiyo, Sirro amewataka wahitimu hao wawe wa kwanza kuonyesha uwezo wao, maadili na wasiwe wa kwanza kuonyesha udhaifu na kutoa mfano wa tukio la askari hao saba.
Septemba 15, 2021 polisi hao wakiwa na gari na silaha walivuka mpaka na kuingia Malawi ambapo walizingirwa na wananchi na kuokolewa na polisi wa nchi hiyo na tayari wamefukuzwa kazi.
“Juzi kuna senior nco (mwenye stesheni sajini) ametoka hapa amekwenda anaongoza askari wanne, watano ni msomi anakimbizana na mtu mwenye magendo na magendo yenyewe hata hayafikii 30, 000."
“Kaingia Malawi kaongoza askari saba anakimbiza magendo anajua amevuka mpaka anakwenda kwenye nchi ya watu wengine na gari ya polisi na silaha ya polisi. Inatupa tabu sana sisi viongozi. Huyu ni msomi ametoka senior NCO hapa anavuka mpaka kwenda nchi ya watu akiwa na silaha ni aibu sana. Ni aibu pia kwetu ambao tunasimamia jeshi,” amesema.
Katika kuweka msisitizo wa suala hilo ameswma, "sitegemei na sitarajii wewe ambaye ni msomi ni inspekta sasa ukaenda kufanya mambo ya hovyo hovyo. Unaweza leo ukafurahia kwamba umepata uinspekta kesho tukachukua uinspekta."
Sirro ameeleza kuwa jeshi hilo linakabiliwa na changamoto ya kufanya upelelezi na kwamba hata Rais Samia Hassan Suluhu amewahi kulizungumza na kuwataka wahakikishe mashauri yanakwisha kwa wakati.
“Tuna challenge (changamoto) kubwa ya upelelezi. Rais amekuwa akisema. Wengine watakwenda kusimamamia madawati ya upelelezi. Wahakikishe mashauri yanakwisha kwa wakati."
“Tuhakikishe mlundikano wa mahabusu unapungua. Mhakikishe haki inatendeka. Hayo ndio maelekezo yangu," amsema Sirro katika hafla hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo.
Kwa upande wake mkuu wa majeshi nchini (CDF), Jenerali Venance Mabeyo amesema kwa sasa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (bila kutaja wapi), linakabiliana na vitisho vya uhuru na mustakabali na usalama wa Tanzania.