- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
GWAJIMA: HAKUNA MKAZI WA KUNDUCHI ATAKAE ONEWA
Mbunge mpya wa jimbo la Kawe, Askofu Josephat Gwajima, amewetaka wakazi waishio maeneo ya Kunduchi jijini Dar es Salaam kuwa na subira na kuwaambia kuwa hakuna mkazi hata mmoja atakaye onewa, wasubiri serikali inaendelea na uchunguzi juu ya eneo lililopatwa na volcano la tope.
Gwajima ametoa kauli hiyo leo Novemba 26, baada ya kutembelea katika eneo hilo lililokumbwa na tope zito la Volcano.
“Wataalam wetu wanaendelea kufanya uchunguzi ili wajue hiki ni kitu gani kama ni mabaidliko ya hali ya hewa au mzunguko wa dunia kwa hiyo tuvute subira wakati serikali inataka kujua tatizo hili jina lake linaitwa nini.
“Tuangalie Serikali inafanya nini katika jambo hili na mimi nitakuwa nao bega kwa bega hakuna mtu atakaye onewa wala kupata shida kwasababu ya jambo hili niwahakikishieni mimi pamoja na wawakilishi wengine tutakuwa pamoja kuona litakalo tokea Kunduchi, niwape pole kwa hili lakini yajayo yanafurahisha," amesema Gwajima.