Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 9:03 pm

ASKOFU ANGLIKANA : MARUFUKU WANASIASA KUSIMAMA MADHABAHUNI KUFANYA SIASA

Kenya. Askofu wa Mkuu wa Kanisa la Kianglikana nchini Kenya Jackson Ole Sapit amepiga marufuku wanasiasa wote nchini Kenya kusimama mbele ya Madhabahu kuhubiri siasa, huku akitanabaisha kuwa wanasiasa wamekiuka utakatifu wa asili wa madhabahu za makanisa.

“Nimepiga marufuku wanasiasa kuongea ndani ya kanisa ya Angliikana,” alisema Askofu Mkuu wa kanisa la Kianglikana nchini Kenya Ole Sapit.

Tangazo hilo lilitolewa kufuatia Askofu wa jimbo Katoliki la Nyeri Anthony Muheria kuwaomba mapadre wa kanisa hilo nchini Kenya ‘’kurejesha madhabahu madhabahu ‘’

Kiongozi wa upinzani ODM Raila Odinga na mwenzake wa chama cha ANC Musalia Mudavadi walikuwa miongoni mwa waathiriwa wa kwanza wa agizo hilo ambapo Jumapili walilazimika kukaa kimya katika sherehe ya kuapishwa kwa Askofu wa kwanza mwanamke wa kanisa hilo iliyofanyika Butere magharibi mwa Kenya.