Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 7:31 am

ZITTO "SEREKALI IMESHINDWA KUTEKELEZA AHADI YA MIL 50 KWA UKOSEFU WA MAARIFA"

MWANZA: Mbunge wa kigoma Mjini na kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe amesema kuwa Serekali ya CCM mwaka 2015 iliahidi wananchi kuwa iwapo itachaguliwa itatekeleza programu ya kutoa milioni 50 kwa kila kijiji programu ambayo serekali imeshindwa kutekeleza, akiongea kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Jana Ijumaa (17.11.2017) katika Kijiji cha Mwamaguha- Kata ya Kijima katika wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza Zitto alisema kuwa hata Rais magufuli mwenyewe amesema kuwa hana pesa hizo.


"Mwaka 2015 CCM iliwaahidi kuwa iwapo itashika madaraka itatekeleza program ya kutoa shilingi 50 milioni kila kijiji nchini, ili zichochee Maendeleo yenu. Halikuwa wazo baya, lakini tulitahadharisha kuwa CCM hawataweza kulitekeleza kwa ufanisi. Machi, 2016 Baraza la Taifa la Uwezeshaji (NEEC) lilitangaza kuwa Serikali imetenga kwenye bajeti shilingi bilioni 800 ili kuanza utekelezaji huo."

"NEEC ilirudia tena tangazo lake hilo mwezi Septemba, 2016 kuwa fedha hizo zitaanza kutolewa mapema mwaka 2017. Mpaka sasa hakuna kijiji kimepata hata senti tano ya mkoloni. alisema Zitto

Katika kugonga msumari wa mwisho kwenye jeneza, juzi Rais Magufuli akiwa hapa Mwanza ametamka rasmi kuwa yeye hana hizo fedha na kwamba anasafisha kwanza ili aweze kuzipata. Kwa hiyo CCM wametoa ahadi isiyotekelezeka. Wamewahadaa nyinyi Wananchi.


Zitto alisema kuwa anajua hali mbaya walizonanazo wananchi kwa sasa,na hali hii imeletwa na serekali ya CCM, nakwmba wasifikiria hali hii mbaya ipo kwao tu " Mnaweza kudhani hali mbaya hii ni kwenu tu, hapana ni nchi nzima hali hiyo, mjini na vijijini watu wote wanalalamika kuwa 'vyuma vimekaza', maisha yamekuwa magumu mno. Na siku hizi sisi ACT Wazalendo tukisema hilo basi Polisi wanatukamata. Uonevu ulioje, Serikali inaua uchumi, tukitumia haki hiyo kusema basi tunakamatwa. Hatutaacha kusema.