Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 1:45 pm

NEWS: BRELA YAENDESHA MAFUNZO KWA VYUO NA TAASISI ZA ELIMU YA JUU.

DODOMA: Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imeendelea na kuendesha mafunzo ya umiliki bunifu wa vyuo na Taasisi za elimu ya juu ikiwemo vyuo vikuu, vyuo vya kati na vyuo vya ufundi stadi lengo likiwa ni kutoa elimu ya miliki bunifu.


Akizungumza leo Jumanne Novemba 26,2024 mara baada ya kuendesha mafunzo katika chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) Afisa usajili kutoka BRELA stanslaus Kigosi amesema wameamua kufanya mafunzo hayo kwenye vyuo kwa kuwa wanaamini kwenye taasisi za elimu pamoja na vyuo vya ufundi ndipo kunapopatikana ubunifu wa kila namna, kwakuwa ndipo walipo watafiti na wanafunzi wanaojifunza, na katika kujifunza kwao wanaibuka na ubunifu wa namna mbalimbali.

"Wakati mwingine wao hawatambui kuwa huo ni ubunifu na ni mali na unaweza kulindwa kwaajili ya kuwaingizia kipato kwa mtu mmoja mmoja na taasisi zao ndio maana sisi leo tumeona tuendeshe mafunzo haya huku" amesema Kigosi.

Naye Mhadhiri kutoka Taasisi za Taaluma na Maendeleo UDOM Benta Matuka amesema kupitia mafunzo hayo wamejifunza mambo mbalimbali yanayohusu BRELA, na kwamba kwa kuwa zamani hakuwa anafahamu taratibu za kufuata pindi mtu akiwa anataka kusajiri biashara yake.

"Kingine nilichojifunza ni kwamba kumbe kusajili shughuli za kitafiti kusajili bidhaa ambazo zimezalishwa zina hatua mbalimbali lakini ni field mbalimbali, na mwanzoni nilikuwa sijui kuhusu copyright kitu gani kiende," elimu niliyoipata hapa itaniwezesha kuwafundisha masuala muhimu namna ya kusajili idea zao walizo zivumbua.

Kwa upande wake Mhitimu wa chuo kikuu cha Dodoma Jospeter Jonathan amesema alianza kujihusisha na bunifu hizo akiwa Mwaka wa kwanza na kupitia mafunzo hayo amefahamu namna gani anaweza kusajili na kumiliki bunifu zake.