- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
ZITTO: KUNA MPANGO WA MUDA KUTAKA KUMUONDOA PROF. ASSAD
Dar es salaam: Mbunge wa Kigoma Ujiji Zitto Kabwe amesema kuwa Kuna mpango wa muda Mrefu sasa wa kutaka kumwondoa kwenye nafasi yake Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serekali CAG Prof. Mussa Assad kwa madai ya kuwa na misimamo mikali juu ya kazi yake hiyo, na hana tabia ya kunyenyekea mamlaka zilizo juu.
" Kikatiba wameshindwa. Walitaraji angetoka Septemba 2019 Lakini Kikatiba haondoki mpaka afike umri wa kustaafu. Wanatafuta njia'' amesema ZittoKauli Zitto inakuja mara baada ya Jana jumatatu Spika wa Bunge wa Tanzania Job Ndugai kumtaka Prof. Assad kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya Bunge siku ya Januari 21, 2019 kwa hiari kwa ajili ya kuhojiwa, vinginevyo atapelekwa kwa pingu kwa Madai ya Kulidhalilisha Bunge.
''Hivi sasa Spika ameagiza Kamati za Bunge za kuisimamia Serikali ( PAC, LAAC, Bajeti na Uwekezaji ) kutofanya kazi na CAG wala maofisa wake. Hii maana yake ni kuwa Bunge halitajadili Taarifa za PAC/LAAC kwenye mkutano ujao wa Bunge ( kukwepa TZS 1.5T ). Hapa Spika anavunja Katiba''
Alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Jana Ndugai alisema Profesa Assad amelidhalilisha Bunge.
Ndugai alisema CAG akiwa nje ya Tanzania wakati anahojiwa na Idhaa ya Kiswahili UN alisema Bunge la Tanzania kuwa ni dhaifu.
"Kama ni upotoshaji basi CAG na ofisi yake ndiyo wapotoshaji, huwezi kusema nchi yako vibaya unapokuwa nje ya nchi, na kwa hili hatuwezi kufanya kazi kwa kuaminiana," amesema Ndugai.
Ndugai alisema kitendo hicho kimemkasirisha kwani hakutegemea msomi kama huyo angeweza kutoa maneno ya kudhalilisha Bunge lililojaa wasomi zaidi ya mabunge yote tangu uhuru.
Mbali na CAG, mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee naye ameitwa mbele ya kamati hiyo siku inayofuata yaani Januari 22, 2019.