- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
ZITTO: BUNGE LIMEJAA WABUNGE WENGI MAKASUKU
Dar es salaam: Mbunge wa Kigoma UJIJI ambae pia ndiyo Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo ameeleza kuwa idadi kubwa ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) bungeni kuna kwamisha maslahi ya wananchi kutokana kutumia wingi wao kupitisha yanayowapendeza watawala wa chama chao.
Vyama Vilivyo shiriki katika mkutano huo ni pamoja na ACT-Wazalendo, Chama cha Wananchi (CUF) Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), NCCR-Mageuzi, NRD, CCK, CHAUMA.
Akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye Ofisi za Chama cha CHAUMA akiambatana na viongozi wa vyama kumi vya upinzani vilivyoungana kutetea demokrasia na kupinga muswada wa sharia ya vyama vya siasa Zitto amesema kuwa muswada wa sheria ya vyombo vya habari utapelekwa bungeni ambapo wabunge wa CCM ambao ndiyo wengi bunge watawashinda wabunge wachache wa upinzani na kupelekea kupita kwa sheria hiyo ya vyama vya siasa ambayo wanaiona ni sheria shetani na ovu kwa demokrasia.
“Bunge limejaa wabunge wa CCM, kuna wabunge wazuri wa chama cha mapinduzi lakini kuna wabunge ‘makasuku’ kiasi kwamba muswada huu ukienda utatoka mbaya zaidi,” amesema Zitto na kuongeza.
“Kuna wabunge wapenda sifa wataufanya muswada huu kuwa mbaya zaidi na tayari tuansikia wapo wabunge watakaopendekeza kwenye sharia hiyo kwamba hakuna kufanya mikutano mpaka uchaguzi hadi uchaguzi.”
Zitto ameeleza kuwa muswada huo uliolenga kuua demokrasia ya kweli ambapo Msajili wa vyama vya siasa atakuwa na mamlaka kamili juu kuingilia mambo ya ndani ya vyama vya siasa.
“Toka ilipoingia madarakani serikali ya awamu ya tano imejipambanua vyema isivyokuwa muumini wa demokrasia, Katiba na hata sheria za nchi yetu, imekuwa serikali inayoongozwa na matamko na kauli kana kwamba nchi iliyotoka vitani
“Itakumbukwa tamko la kuzuia vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara lilitolewa na Rais John Magufuli wakati anahutubia wanachama wa CCM Mkoani Singida mwaka 2016, tamko hilo lilikuwa kinyume cha katiba na sheria za nchi ambapo linaendelea kushikiwa bango na vyombo ya ulinzi na usalama kwa kuwabana wapinzani wakati chama tawala kikiendelea na shughuli zake za kisiasa mahali popote bila pingamizi,” amesema Zitto.