- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
WAZIRI SHONZA: WEMA HANA UTOTO WOWOTE, ASUBIRI ADHABU TU
Dar es Salaam: Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amekataa kukubali utetezi wa Msanii wa Bongo Move Wema Sepetu kwamba kosa alilofanya linatokana na utoto ambapo kiuhalisia sio kweli.
Shonza amesema Wema anamiaka 30 sawa na yeye mwenye miaka 31, tatizo lake ameshindwa kujitambua kuwa yeye ni nani kwenye jamii.
“Wema hana utoto wowote, miaka 30 ukaseme mtoto, mie nina miaka 31 mbona sifanyi vitu kama hivyo na sijawahi kufanya,” amesema Shonza
Kufuatia hilo, amesema wizara kama mlezi wa wasanii itahakikisha inakemea vitendo hivyo na kuchukua hatua stahiki kwa wahusika wanaoitia doa tasnia ya sanaa.
“Bodi ya filamu imeshachukua hatua lakini bado mamlaka nyingine zitatekeleza majukumu yake katika hilo, asubiri adhabu ya (Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) ,” amesema.
Hilo linaungwa mkono na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata), Godfrey Mngereze ambaye amesema vitendo vichafu vya Wema vinajirudia mara kwa mara.
Msanii huyo juzi Alhamisi aliomba radhi kufuatia kusambaa kwa picha zake za faragha na Bodi ya Filamu Tanzania imemfungia kujihusisha na masuala ya filamu na uigizaji kwa muda usiojulikana.