Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 3:37 am

WAZIRI MWIJAGE: KAMA HAUNA TAX CLEARENCE HAUPATI MCHUMBA

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage ametahadharisha kuwa, wasiokuwa na utamaduni wa kulipa kodi yanaweza kuwakuta aliyoyaona kwenye nchi nyingine, ya kunyimwa mchumba baada ya kukosa Tax Clearence

“Tunataka ifikapo mwisho wa mwezi watu kwa mapenzi yao waende kulipa kodi, yasije kuwakuta niliyo ona kwenye nchi fulani, unakwenda kuchumbia wanakuomba ‘tax clearence’, kama huna ‘tax clearence’ mchumba hupati,” amesema Waziri Mwijage

Waziri Mwijage amesema hayo katika sherehe ya uzinduzi wa maonesho ya bidhaa zinazotengenezwa na viwanda vya mkoa wa Pwani, iliyofanyika leo tarehe 29 Oktoba 2018, wilayani Kibaha mkoani humo.

Katika hatua nyingine, Waziri Mwijage amesema serikali imedhamiria kujenga uchumi wa kitaifa ili ifikapo mwaka 2025 kipato cha mtanzania kiwe dola za Marekani 3,000 pamoja na kuwa na taifa la watu walioelimika na wepesi wa kujifunza.

“Tanzania tunajenga uchumi wa kitaifa sio uchumi wa taifa, ni uchumi wa kitaifa, ifikapo 2025 wastani wa kipato cha mtanzania katika huo uchumi wa kitaifa iwe dola 3000, kwa kila mtu kama milioni 7.5, lakini vile vile kufika 2025 tuwe na taifa la watu walioelimika na wepesi wa kujifunza,” amesema na kuongeza Waziri Mwijage.

“Tunataka katika huo uchumi wa kitaifa tuendelee kuwa na utulivu na mshikamano, tujenge taifa lenye utawala bora, ukizungumza utawala bora watu wanaiangilia serikali, hapana hata kutotii sheria ina maana na wewe huna utawala bora.”