- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
UTAFITI: TATIZO LA MTU MZIMA KUKOJOA KITANDANI
Hii ni hali ya kukojoa kitandani wakati mtu amelala, tatizo hili linapotokea kwa mtoto wa chini ya miaka sita sio ugonjwa na mara nyingi huisha lenyewe.
Watoto wengine huendelea kukojoa kitandani mpaka umri wa kubalehe na kuvunja ungo. Lakini tatizo hili hupotea anapokua mtu mzima kabisa.
Sababu kwanini mtoto anayeweza kukojoa mwenyewe mchana kuendelea kukojoa wakati amesinzia haileweki , mara nyingi watoto wa kiume hujikojolea sana kuliko wa kike lakini kuna mahusiano ya kurithi tatizo hili yaani kuna uwezekano mkubwa baba wa mtoto au mama alikuaga kikojozi pia kwenye utoto wake.
Kwa watu wazima tatizo la kukojoa kitandani hua ni ugonjwa flani. Mfano wa magonjwa haya ni,
Kisukari{diabetes mellitus}:
Ugonjwa huu huambatana na dalili ya kupata kiu sana, njaa kali na kwenda kukojoa mara kwa marawakati wa usiku.
Magonjwa ya njia ya mkojo{chronic urinary tract infection}:
Hii ni kutokana na kuharibika kwa kibofu cha mkojo ambacho ni muhimu katika kutambua ujazo wa flani wa mkojo ili mtu aende kukojoa hivyo kuugua kwa kibofu husababisha kisifanye kazi vizuri. mfano cystitis
Magonjwa au kuumia kwa mishipa ya fahamu:{ structural or infections of nerves}
Mishipa ya fahamu ni muhimu katika kutoa taarifa za ujazo wa mkojo kwenye kibofu. Kibofu kinapofikisha ujazo wa 300mils mpaka 400mils taarifa hutumwa kwenye ubongo, kisha ubongo hurudisha taarifa za kuruhusu mtu akojoe. Kuharibika kwa mishipa hii ya fahamu husababisha kujikojolea mfano kuvunjika kiuno, kiharusi, magojwa ya akili, multiple sclerosis na alzeheimers disease.
Kuvimba kwa tezi dume{prostate enlargement}:
Tezi dume ni kiungo kinachopitiwa katikati na mirija ya mkojo{urethra}, hivyo kuvimba kwake hubana mirija hiyo na kusababisha kukojoa mara kwa mara[incontinence}.
Vipimo ambavyo hupimwa mahospitalini:
- Kupima mkojo kuangalia kama kuna shida yeyote ya mfumo huo.
- Kupima mkunduni kama tezi dume imevimba.{digital rectal examination}
- X-ray kuangalia kama kuna tatizo la umbo la kibofu cha mkojo.
- MATIBABU…
- kutibu chanzo cha tatizo ni njia nzuri zaidi.. mfano
- Antibiotics mfano cotrimoxazole hutolewa kama tatizo la mfumo wa mkojo i.e UTIs
- Anticholinergic mfano colirem hutolewa kwa matatizo ya mishipa ya fahamu.
- Upasuaji hufanyika kwa uvimbe wa tezi dume.{prostate}
- Kufuata sheria na matibabu ya kisukari itakusaidia kupunguza shida hiyo.
- MATIBABU MENGINE….
- Kama mtoto anakojoa kitandani acha kumuaibisha na kumtukana mbele za watu ila mpe zawadi pale anapoamka asubuhi bila kukojoa.
- Kama unakojoa kitandani kunywa vinywaji mchana na usiku usitumie kinywaji chochote.
- Aina flani za vyakula na vinywaji humfanya mtu akojoe mara kwa mara sio vizuri kutumia kama ww ni muhanga. Mfano kahawa, pombeau chai.
- Kama unatumia aina ya dawa kikundi cha diuretics kutibu ugonjwa wowote ule mfano furasamide ongea na doctor wako akubadilishie kwan dawa hizo humfanya mtu akojoe sana.
- Kuna pedi maalumu kwa wanaume wanaojikojolea ambazo zinatakiwa zishikwe na chupi ila hazipatikani kirahisi nchini kwetu.
- Mwisho ni vizuri kuoga mapema na kufua mashuka iwapo umejikuta umejikojolea ili kulinda ngozi yako. bonyeza hpa kusoma zaidi
angalizo; kwanzia sasa, ushauri wowote kutoka kwa daktari, wa matatizo binafsi kwa njia ya simu utatozwa shilingi 5000, ushauri kwa kufika ofisini kwetu gongo la mboto dar es laam utatozwa shilingi 10000.malipo hayo yatafanywa kwa namba hizo hapo juu.karibuni sana...